Translate

Monday, July 15, 2013

Cesc Fabregas Kurudi Uingereza?

Kwa Mujibu wa Sky Sport News,Manchester United Imeweka Mezani ofa ya Pauni Milioni 25 ili kumrudisha Cesc Fabregas Uingereza.

Kiungo huyo wa Barcelona mara nyingi Alirudia kusema kuwa anahitaji kupumzika katika klabu yake hiyo ya Nyumbani.

Huu ni mwaka wake wa  pili tangu arudi Katarunya akitokea Arsenal.

Ofa ya Manchester United inaweza ikawa ni ya chini  ukilinganisha thamani ya timu ya Barcelona ndani ya Timu ya Taifa ya Hispania


Manchester United wapo katika harakati za kupata kiungo mbunifu ili kuziba pengo la Paul Scholes ambaye alistaafu mwishoni mwa msimu uliokwisha,na inaonekana Cesc Fabregas anafaa kuziba pengo hilo.

Kama Manchester United itafanikiwa kumnasa kiungo huyo,atakuwa ni kapteni wa pili kutokea Arsenal na kujiunga Manchester United baada ya Robin Van Persie.

http://www1.skysports.com/football/news/11667/8825456/Transfer-news-Manchester-United-make-25m-offer-for-Barcelona-s-Cesc-Fabregas


No comments:

Post a Comment